___Translations___

_Quran?_

_Gadgets_

_Search_

_Links_

_Contribute_

_Note_

1 - AL-FAATIH'A
2 - AL - BAQARA
3 - AL I'MRAN
4 - AN-NISAAI
5 - AL - MAIDA
6 - AL - AN-A'AM
7 - AL - A'RAAF
8 - AL - ANFAAL
9 - AT-TAWBA
10 - YUNUS
11 - HUD
12 - YUSUF
13 - AR-RAA'D
14 - IBRAHIM
15 - AL - HIJR
16 - AN NAH'L
17 - AL ISRAAI (BANI ISRAIL)
18 - AL - KAHF
19 - MARYAM
20 - T'AHA
21 - AL - ANBIYAA
22 - AL -HAJJ
23 - AL - MUUMINUN
24 - AN - NUR
25 - AL - FURQAN
26 - ASH-SHUA'RAA
27 - AN-NAML
28 - AL-QAS'AS'
29 - AL - A'NKABUT
30 - AR-RUM
31 - LUQMAN
32 - ASSAJDAH
33 - AL-AH'ZAB
34 - SABAA
35 - FAAT'IR
36 - YA-SIN
37 - ASS'AFFAT
38 - S'AAD
39 - AZZUMAR
40 - GHAAFIR (AU AL MUUMIN)
41 - FUSS'ILAT (AU H'A MIM SAJDAH)
42 - ASH-SHUURA
43 - AZZUKHRUF
44 - ADDUKHAN
45 - AL - JAATHIYA
46 - AL - AH'QAAF
47 - MUH'AMMAD
48 - AL FAT-H'I
49 - AL H'UJURAAT
50 - QAAF
51 - ADH-DHAARIYAAT
52 - ATT'UR
53 - ANNAJM
54 - AL-QAMAR
55 - ARRAH'MAN
56 - AL -WAAQIA'H
57 - AL -H'ADIID
58 - AL - MUJAADALAH
59 - AL - H'ASHRI
60 - AL - MUMTAH'INAH
61 - ASS'AF
62 - AL - JUMUA'
63 - AL - MUNAAFIQUN
64 - ATTAGHAABUN
65 - ATT'ALAAQ
66 - ATTAH'RIIM
67 - AL - MULK
68 - AL - QALAM
69 - AL - H'AAQQAH
70 - AL - MAA'RIJ
71 - NUH'
72 - AL - JINN
73 - AL - MUZZAMMIL
74 - AL - MUDDATHTHIR
75 - AL - QIYAMAH
76 - AL - INSAN
77 - AL - MURSALAAT
78 - ANNABAA
79 - ANNAZIA'AT
80 - A'BASA
81 - ATTAKWIR
82 - AL - INFIT'AAR
83 - AL - MUT'AFFIFIIN
84 - AL - INSHIQAAQ
85 - AL - BURUUJ
86 - ATT'AARIQ
87 - AL - AA'LAA
88 - AL - GHAASHIYAH
89 - AL - FAJR
90 - AL - BALAD
91 - ASH-SHAMS
92 - AL - LAYL
93 - WADH-DHUH'AA
94 - ASH-SHARH'
95 - AT-TIN
96 - AL - A'LAQ
97 - AL - QADR
98 - AL - BAYYINAH
99 - AZ-ZILZALAH
100 - AL - A'ADIYAAT
101 - AL - QAARIA'H
102 - AT-TAKAATHUR
103 - AL - A'S'R
104 - AL - HUMAZAH
105 - AL - FIIL
106 - QURAISH
107 - AL - MAAU'N
108 - AL - KAWTHAR
109 - AL - KAFIRUN
110 - ANNAS'R
111 - AL - MASAD
112 - AL - IKHLAS'
113 - AL - FALAQ
114 - ANNAS
KISWAHILI

77 - AL - MURSALAAT

 

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole!
 
2Na zinazo vuma kwa kasi!
 
3Na zikaeneza maeneo yote!
 
4Na zinazo farikisha zikatawanya!
 
5Na zinazo peleka mawaidha!
 
6Kwa kuudhuru au kuonya,
 
7Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa!
 
8Wakati nyota zitakapo futwa,
 
9Na mbingu zitakapo pasuliwa,
 
10Na milima itakapo peperushwa,
 
11Na Mitume watakapo wekewa wakati wao,
 
12Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?
 
13Kwa siku ya kupambanua!
 
14Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini?
 
15Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha!
 
16Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia?
 
17Kisha tukawafuatilizia walio fuatia?
 
18Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu!
 
19Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
 
20Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?
 
21Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?
 
22Mpaka muda maalumu?
 
23Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.
 
24Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
 
25Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya
 
26Walio hai na maiti?
 
27Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu?
 
28Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
 
29Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha!
 
30Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!
 
31Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.
 
32Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!
 
33Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!
 
34Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
 
35Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu,
 
36Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.
 
37Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
 
38Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia.
 
39Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!
 
40Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
 
41Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem,
 
42Na matunda wanayo yapenda,
 
43Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda.
 
44Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema.
 
45Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
 
46Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!
 
47Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
 
48Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami.
 
49Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
 
50Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?