___Translations___

_Quran?_

_Gadgets_

_Search_

_Links_

_Contribute_

_Note_

1 - AL-FAATIH'A
2 - AL - BAQARA
3 - AL I'MRAN
4 - AN-NISAAI
5 - AL - MAIDA
6 - AL - AN-A'AM
7 - AL - A'RAAF
8 - AL - ANFAAL
9 - AT-TAWBA
10 - YUNUS
11 - HUD
12 - YUSUF
13 - AR-RAA'D
14 - IBRAHIM
15 - AL - HIJR
16 - AN NAH'L
17 - AL ISRAAI (BANI ISRAIL)
18 - AL - KAHF
19 - MARYAM
20 - T'AHA
21 - AL - ANBIYAA
22 - AL -HAJJ
23 - AL - MUUMINUN
24 - AN - NUR
25 - AL - FURQAN
26 - ASH-SHUA'RAA
27 - AN-NAML
28 - AL-QAS'AS'
29 - AL - A'NKABUT
30 - AR-RUM
31 - LUQMAN
32 - ASSAJDAH
33 - AL-AH'ZAB
34 - SABAA
35 - FAAT'IR
36 - YA-SIN
37 - ASS'AFFAT
38 - S'AAD
39 - AZZUMAR
40 - GHAAFIR (AU AL MUUMIN)
41 - FUSS'ILAT (AU H'A MIM SAJDAH)
42 - ASH-SHUURA
43 - AZZUKHRUF
44 - ADDUKHAN
45 - AL - JAATHIYA
46 - AL - AH'QAAF
47 - MUH'AMMAD
48 - AL FAT-H'I
49 - AL H'UJURAAT
50 - QAAF
51 - ADH-DHAARIYAAT
52 - ATT'UR
53 - ANNAJM
54 - AL-QAMAR
55 - ARRAH'MAN
56 - AL -WAAQIA'H
57 - AL -H'ADIID
58 - AL - MUJAADALAH
59 - AL - H'ASHRI
60 - AL - MUMTAH'INAH
61 - ASS'AF
62 - AL - JUMUA'
63 - AL - MUNAAFIQUN
64 - ATTAGHAABUN
65 - ATT'ALAAQ
66 - ATTAH'RIIM
67 - AL - MULK
68 - AL - QALAM
69 - AL - H'AAQQAH
70 - AL - MAA'RIJ
71 - NUH'
72 - AL - JINN
73 - AL - MUZZAMMIL
74 - AL - MUDDATHTHIR
75 - AL - QIYAMAH
76 - AL - INSAN
77 - AL - MURSALAAT
78 - ANNABAA
79 - ANNAZIA'AT
80 - A'BASA
81 - ATTAKWIR
82 - AL - INFIT'AAR
83 - AL - MUT'AFFIFIIN
84 - AL - INSHIQAAQ
85 - AL - BURUUJ
86 - ATT'AARIQ
87 - AL - AA'LAA
88 - AL - GHAASHIYAH
89 - AL - FAJR
90 - AL - BALAD
91 - ASH-SHAMS
92 - AL - LAYL
93 - WADH-DHUH'AA
94 - ASH-SHARH'
95 - AT-TIN
96 - AL - A'LAQ
97 - AL - QADR
98 - AL - BAYYINAH
99 - AZ-ZILZALAH
100 - AL - A'ADIYAAT
101 - AL - QAARIA'H
102 - AT-TAKAATHUR
103 - AL - A'S'R
104 - AL - HUMAZAH
105 - AL - FIIL
106 - QURAISH
107 - AL - MAAU'N
108 - AL - KAWTHAR
109 - AL - KAFIRUN
110 - ANNAS'R
111 - AL - MASAD
112 - AL - IKHLAS'
113 - AL - FALAQ
114 - ANNAS
KISWAHILI

51 - ADH-DHAARIYAAT

 

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1Naapa kwa pepo zinazo tawanya,
 
2Na zinazo beba mizigo,
 
3Na zinazo kwenda kwa wepesi.
 
4Na zinazo gawanya kwa amri,
 
5Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli,
 
6Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea.
 
7Naapa kwa mbingu zenye njia,
 
8Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo khitalifiana.
 
9Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa.
 
10Wazushi wameangamizwa.
 
11Ambao wameghafilika katika ujinga.
 
12Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo?
 
13Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni.
 
14Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza.
 
15Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem.
 
16Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema.
 
17Walikuwa wakilala kidogo tu usiku.
 
18Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira.
 
19Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba.
 
20Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini.
 
21Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni?
 
22Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa.
 
23Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema.
 
24Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa?
 
25Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni.
 
26Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona.
 
27Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli?
 
28Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu.
 
29Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa!
 
30Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua.
 
31AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa?
 
32Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu,
 
33Tuwatupie mawe ya udongo,
 
34Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka.
 
35Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini.
 
36Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu!
 
37Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu.
 
38Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi.
 
39Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu!
 
40Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa.
 
41Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa kukata uzazi.
 
42Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya kama kilio nyambuka.
 
43Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu.
 
44Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona.
 
45Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea.
 
46Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu.
 
47Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua.
 
48Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi!
 
49Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie.
 
50Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
 
51Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
 
52Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu.
 
53Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi.
 
54Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi.
 
55Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.
 
56Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.
 
57Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe.
 
58Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti.
 
59Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasinihimize.
 
60Ole wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa.