___Translations___

_Quran?_

_Gadgets_

_Search_

_Links_

_Contribute_

_Note_

1 - AL-FAATIH'A
2 - AL - BAQARA
3 - AL I'MRAN
4 - AN-NISAAI
5 - AL - MAIDA
6 - AL - AN-A'AM
7 - AL - A'RAAF
8 - AL - ANFAAL
9 - AT-TAWBA
10 - YUNUS
11 - HUD
12 - YUSUF
13 - AR-RAA'D
14 - IBRAHIM
15 - AL - HIJR
16 - AN NAH'L
17 - AL ISRAAI (BANI ISRAIL)
18 - AL - KAHF
19 - MARYAM
20 - T'AHA
21 - AL - ANBIYAA
22 - AL -HAJJ
23 - AL - MUUMINUN
24 - AN - NUR
25 - AL - FURQAN
26 - ASH-SHUA'RAA
27 - AN-NAML
28 - AL-QAS'AS'
29 - AL - A'NKABUT
30 - AR-RUM
31 - LUQMAN
32 - ASSAJDAH
33 - AL-AH'ZAB
34 - SABAA
35 - FAAT'IR
36 - YA-SIN
37 - ASS'AFFAT
38 - S'AAD
39 - AZZUMAR
40 - GHAAFIR (AU AL MUUMIN)
41 - FUSS'ILAT (AU H'A MIM SAJDAH)
42 - ASH-SHUURA
43 - AZZUKHRUF
44 - ADDUKHAN
45 - AL - JAATHIYA
46 - AL - AH'QAAF
47 - MUH'AMMAD
48 - AL FAT-H'I
49 - AL H'UJURAAT
50 - QAAF
51 - ADH-DHAARIYAAT
52 - ATT'UR
53 - ANNAJM
54 - AL-QAMAR
55 - ARRAH'MAN
56 - AL -WAAQIA'H
57 - AL -H'ADIID
58 - AL - MUJAADALAH
59 - AL - H'ASHRI
60 - AL - MUMTAH'INAH
61 - ASS'AF
62 - AL - JUMUA'
63 - AL - MUNAAFIQUN
64 - ATTAGHAABUN
65 - ATT'ALAAQ
66 - ATTAH'RIIM
67 - AL - MULK
68 - AL - QALAM
69 - AL - H'AAQQAH
70 - AL - MAA'RIJ
71 - NUH'
72 - AL - JINN
73 - AL - MUZZAMMIL
74 - AL - MUDDATHTHIR
75 - AL - QIYAMAH
76 - AL - INSAN
77 - AL - MURSALAAT
78 - ANNABAA
79 - ANNAZIA'AT
80 - A'BASA
81 - ATTAKWIR
82 - AL - INFIT'AAR
83 - AL - MUT'AFFIFIIN
84 - AL - INSHIQAAQ
85 - AL - BURUUJ
86 - ATT'AARIQ
87 - AL - AA'LAA
88 - AL - GHAASHIYAH
89 - AL - FAJR
90 - AL - BALAD
91 - ASH-SHAMS
92 - AL - LAYL
93 - WADH-DHUH'AA
94 - ASH-SHARH'
95 - AT-TIN
96 - AL - A'LAQ
97 - AL - QADR
98 - AL - BAYYINAH
99 - AZ-ZILZALAH
100 - AL - A'ADIYAAT
101 - AL - QAARIA'H
102 - AT-TAKAATHUR
103 - AL - A'S'R
104 - AL - HUMAZAH
105 - AL - FIIL
106 - QURAISH
107 - AL - MAAU'N
108 - AL - KAWTHAR
109 - AL - KAFIRUN
110 - ANNAS'R
111 - AL - MASAD
112 - AL - IKHLAS'
113 - AL - FALAQ
114 - ANNAS
KISWAHILI

53 - ANNAJM

 

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1Naapa kwa nyota inapo tua,
 
2Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea.
 
3Wala hatamki kwa matamanio.
 
4Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa;
 
5Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu,
 
6Mwenye kutua, akatulia,
 
7Naye yuko juu kabisa upeo wa macho.
 
8Kisha akakaribia na akateremka.
 
9Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi.
 
10Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alicho mfunulia.
 
11Moyo haukusema uwongo uliyo yaona.
 
12Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona?
 
13Na akamwona mara nyingine,
 
14Penye Mkunazi wa mwisho.
 
15Karibu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa.
 
16Kilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika.
 
17Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka.
 
18Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi.
 
19Je! Mmemuona Lata na Uzza?
 
20Na Manaat, mwingine wa tatu?
 
21Je! Nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake?
 
22Huo ni mgawanyo wa dhulma!
 
23Hayo hayakuwa ila ni majina mliyo wapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi.
 
24Ati mtu anakipata kila anacho kitamani?
 
25Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera.
 
26Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipo kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia.
 
27Hakika wasio amini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike.
 
28Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki.
 
29Basi mwachilie mbali anaye upa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia.
 
30Huo ndio mwisho wao wa ujuzi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuongoka.
 
31Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, ili awalipe walio tenda ubaya kwa waliyo yatenda, na walio tenda mema awalipe mema.
 
32Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu.
 
33Je! Umemwona yule aliye geuka?
 
34Na akatoa kidogo, kisha akajizuia?
 
35Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona?
 
36Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa?
 
37Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi?
 
38Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine?
 
39Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe?
 
40Na kwamba vitendo vyake vitaonekana?
 
41Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu.
 
42Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho.
 
43Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio.
 
44Na kwamba Yeye ndiye anaye fisha na kuhuisha.
 
45Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike
 
46Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa.
 
47Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine.
 
48Na kwamba ni Yeye ndiye anaye tosheleza na kukinaisha.
 
49Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra.
 
50Na kwamba Yeye ndiye aliye waangamiza A'di wa kwanza,
 
51Na Thamudi hakuwabakisha,
 
52Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhaalimu zaidi, na waovu zaidi;
 
53Na miji iliyo pinduliwa, ni Yeye aliye ipindua.
 
54Vikaifunika vilivyo funika.
 
55Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayo ifanyia shaka?
 
56Hili ni Onyo katika maonyo yale yale ya zamani.
 
57Kiyama kimekaribia!
 
58Hapana wa kukifichua isipo kuwa Mwenyezi Mungu.
 
59Je! Mnayastaajabia maneno haya?
 
60Na mnacheka, wala hamlii?
 
61Nanyi mmeghafilika?
 
62Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu.