Translations Suras
KISWAHILI

107 - AL - MAAU'N

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo?
 
2Huyo ndiye anaye msukuma yatima,
 
3Wala hahimizi kumlisha masikini.
 
4Basi, ole wao wanao sali,
 
5Ambao wanapuuza Sala zao;
 
6Ambao wanajionyesha,
 
7Nao huku wanazuia msaada.
 
 
ReadTheQuran.org