Translations Suras
KISWAHILI

105 - AL - FIIL

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo?
 
2Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?
 
3Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi,
 
4Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni,
 
5Akawafanya kama majani yaliyo liwa!
 
 
ReadTheQuran.org