| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
104 - AL - HUMAZAH | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Ole wake kila safihi, msengenyaji! |
| 2 | Aliye kusanya mali na kuyahisabu. |
| 3 | Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele! |
| 4 | Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama. |
| 5 | Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama? |
| 6 | Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa. |
| 7 | Ambao unapanda nyoyoni. |
| 8 | Hakika huo utafungiwa nao |
| 9 | Kwenye nguzo zilio nyooshwa. |
| ReadTheQuran.org | |