| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
101 - AL - QAARIA'H | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Inayo gonga! |
| 2 | Nini Inayo gonga? |
| 3 | Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga? |
| 4 | Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika; |
| 5 | Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa! |
| 6 | Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, |
| 7 | Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza. |
| 8 | Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, |
| 9 | Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya! |
| 10 | Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo? |
| 11 | Ni Moto mkali! |
| ReadTheQuran.org | |