Translations Suras
KISWAHILI

100 - AL - A'ADIYAAT

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
 
2Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
 
3Wakishambulia wakati wa asubuhi,
 
4Huku wakitimua vumbi,
 
5Na wakijitoma kati ya kundi,
 
6Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!
 
7Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!
 
8Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!
 
9Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
 
10Na yakakusanywa yaliomo vifuani?
 
11Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!
 
 
ReadTheQuran.org