| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
99 - AZ-ZILZALAH | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake! |
| 2 | Na itakapo toa ardhi mizigo yake! |
| 3 | Na mtu akasema: Ina nini? |
| 4 | Siku hiyo itahadithia khabari zake. |
| 5 | Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia! |
| 6 | Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao! |
| 7 | Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! |
| 8 | Na anaye tenda chembe ya uovu atauona! |
| ReadTheQuran.org | |