Translations Suras
KISWAHILI

97 - AL - QADR

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu.
 
2Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri?
 
3Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.
 
4Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo.
 
5Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.
 
 
ReadTheQuran.org