| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
96 - AL - A'LAQ | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, |
| 2 | Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, |
| 3 | Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! |
| 4 | Ambaye amefundisha kwa kalamu. |
| 5 | Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui. |
| 6 | Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri |
| 7 | Akijiona katajirika. |
| 8 | Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo. |
| 9 | Umemwona yule anaye mkataza |
| 10 | Mja anapo sali? |
| 11 | Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu? |
| 12 | Au anaamrisha uchamngu? |
| 13 | Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma? |
| 14 | Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona? |
| 15 | Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele! |
| 16 | Shungi la uwongo, lenye makosa! |
| 17 | Basi na awaite wenzake! |
| 18 | Nasi tutawaita Mazabania! |
| 19 | Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee! |
| ReadTheQuran.org | |