| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
94 - ASH-SHARH' | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Hatukukunjulia kifua chako? |
| 2 | Na tukakuondolea mzigo wako, |
| 3 | Ulio vunja mgongo wako? |
| 4 | Na tukakunyanyulia utajo wako? |
| 5 | Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi, |
| 6 | Hakika pamoja na uzito upo wepesi. |
| 7 | Na ukipata faragha, fanya juhudi. |
| 8 | Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie. |
| ReadTheQuran.org | |