| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
93 - WADH-DHUH'AA | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Naapa kwa mchana! |
| 2 | Na kwa usiku unapo tanda! |
| 3 | Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. |
| 4 | Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. |
| 5 | Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. |
| 6 | Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi? |
| 7 | Na akakukuta umepotea akakuongoa? |
| 8 | Akakukuta mhitaji akakutosheleza? |
| 9 | Basi yatima usimwonee! |
| 10 | Na anaye omba au kuuliza usimkaripie! |
| 11 | Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie. |
| ReadTheQuran.org | |