| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
92 - AL - LAYL | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Naapa kwa usiku unapo funika! |
| 2 | Na mchana unapo dhihiri! |
| 3 | Na kwa Aliye umba dume na jike! |
| 4 | Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali. |
| 5 | Ama mwenye kutoa na akamchamngu, |
| 6 | Na akaliwafiki lilio jema, |
| 7 | Tutamsahilishia yawe mepesi. |
| 8 | Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake, |
| 9 | Na akakanusha lilio jema, |
| 10 | Tutamsahilishia yawe mazito! |
| 11 | Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia? |
| 12 | Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu. |
| 13 | Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia. |
| 14 | Basi nakuonyeni na Moto unao waka! |
| 15 | Hatauingia ila mwovu kabisa! |
| 16 | Anaye kadhibisha na kupa mgongo. |
| 17 | Na mchamngu ataepushwa nao, |
| 18 | Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa. |
| 19 | Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa. |
| 20 | Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa. |
| 21 | Naye atakuja ridhika! |
| ReadTheQuran.org | |