Translations Suras
KISWAHILI

91 - ASH-SHAMS

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1Naapa kwa jua na mwangaza wake!
 
2Na kwa mwezi unapo lifuatia!
 
3Na kwa mchana unapo lidhihirisha!
 
4Na kwa usiku unapo lifunika!
 
5Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga!
 
6Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza!
 
7Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza!
 
8Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake,
 
9Hakika amefanikiwa aliye itakasa,
 
10Na hakika amekhasiri aliye iviza.
 
11Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao,
 
12Alipo simama mwovu wao mkubwa,
 
13Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake.
 
14Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa.
 
15Wala Yeye haogopi matokeo yake.
 
 
ReadTheQuran.org