| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
90 - AL - BALAD | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Naapa kwa Mji huu! |
| 2 | Nawe unaukaa Mji huu. |
| 3 | Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa. |
| 4 | Hakika tumemuumba mtu katika taabu. |
| 5 | Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza? |
| 6 | Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. |
| 7 | Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona? |
| 8 | Kwani hatukumpa macho mawili? |
| 9 | Na ulimi, na midomo miwili? |
| 10 | Na tukambainishia zote njia mbili? |
| 11 | Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. |
| 12 | Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? |
| 13 | Kumkomboa mtumwa; |
| 14 | Au kumlisha siku ya njaa |
| 15 | Yatima aliye jamaa, |
| 16 | Au masikini aliye vumbini. |
| 17 | Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. |
| 18 | Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. |
| 19 | Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. |
| 20 | Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande. |
| ReadTheQuran.org | |