| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
89 - AL - FAJR | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Naapa kwa alfajiri, |
| 2 | Na kwa masiku kumi, |
| 3 | Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja, |
| 4 | Na kwa usiku unapo pita, |
| 5 | Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili? |
| 6 | Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di? |
| 7 | Wa Iram, wenye majumba marefu? |
| 8 | Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi? |
| 9 | Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni? |
| 10 | Na Firauni mwenye vigingi? |
| 11 | Ambao walifanya jeuri katika nchi? |
| 12 | Wakakithirisha humo ufisadi? |
| 13 | Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu. |
| 14 | Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia. |
| 15 | Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu! |
| 16 | Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge! |
| 17 | Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima, |
| 18 | Wala hamhimizani kulisha masikini; |
| 19 | Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa, |
| 20 | Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi. |
| 21 | Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande, |
| 22 | Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu, |
| 23 | Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini? |
| 24 | Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu! |
| 25 | Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake. |
| 26 | Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake. |
| 27 | Ewe nafsi iliyo tua! |
| 28 | Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha. |
| 29 | Basi ingia miongoni mwa waja wangu, |
| 30 | Na ingia katika Pepo yangu. |
| ReadTheQuran.org | |