Translations Suras
KISWAHILI

88 - AL - GHAASHIYAH

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?
 
2Siku hiyo nyuso zitainama,
 
3Zikifanya kazi, nazo taabani.
 
4Ziingie katika Moto unao waka -
 
5Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka.
 
6Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba.
 
7Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.
 
8Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.
 
9Zitakuwa radhi kwa juhudi yao,
 
10Katika Bustani ya juu.
 
11Hawatasikia humo upuuzi.
 
12Humo imo chemchem inayo miminika.
 
13Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa,
 
14Na bilauri zilizo pangwa,
 
15Na matakia safu safu,
 
16Na mazulia yaliyo tandikwa.
 
17Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?
 
18Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?
 
19Na milima jinsi ilivyo thibitishwa?
 
20Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?
 
21Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
 
22Wewe si mwenye kuwatawalia.
 
23Lakini anaye rudi nyuma na kukataa,
 
24Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!
 
25Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.
 
26Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!
 
 
ReadTheQuran.org