Translations Suras
KISWAHILI

87 - AL - AA'LAA

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa,
 
2Aliye umba, na akaweka sawa,
 
3Na ambaye amekadiria na akaongoa,
 
4Na aliye otesha malisho,
 
5Kisha akayafanya makavu, meusi.
 
6Tutakusomesha wala hutasahau,
 
7Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.
 
8Na tutakusahilishia yawe mepesi.
 
9Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.
 
10Atakumbuka mwenye kuogopa.
 
11Na atajitenga mbali nayo mpotovu,
 
12Ambaye atauingia Moto mkubwa.
 
13Tena humo hatakufa wala hawi hai.
 
14Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa.
 
15Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.
 
16Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!
 
17Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.
 
18Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,
 
19Vitabu vya Ibrahimu na Musa.
 
 
ReadTheQuran.org