| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
86 - ATT'AARIQ | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku! |
| 2 | Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku? |
| 3 | Ni Nyota yenye mwanga mkali. |
| 4 | Hapana nafsi ila inayo mwangalizi. |
| 5 | Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani? |
| 6 | Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa, |
| 7 | Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu. |
| 8 | Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha. |
| 9 | Siku zitakapo dhihirishwa siri. |
| 10 | Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi. |
| 11 | Naapa kwa mbingu yenye marejeo! |
| 12 | Na kwa ardhi inayo pasuka! |
| 13 | Hakika hii ni kauli ya kupambanua. |
| 14 | Wala si mzaha. |
| 15 | Hakika wao wanapanga mpango. |
| 16 | Na Mimi napanga mpango. |
| 17 | Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole. |
| ReadTheQuran.org | |