| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
85 - AL - BURUUJ | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Naapa kwa mbingu yenye Buruji! |
| 2 | Na kwa siku iliyo ahidiwa! |
| 3 | Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa! |
| 4 | Wameangamizwa watu wa makhandaki |
| 5 | Yenye moto wenye kuni nyingi, |
| 6 | Walipo kuwa wamekaa hapo, |
| 7 | Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini. |
| 8 | Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa, |
| 9 | Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu. |
| 10 | Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua. |
| 11 | Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa. |
| 12 | Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali. |
| 13 | Yeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejeza tena, |
| 14 | Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi, |
| 15 | Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu, |
| 16 | Atendaye ayatakayo. |
| 17 | Je! Zimekuwasilia khabari za majeshi? |
| 18 | Ya Firauni na Thamudi? |
| 19 | Lakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha. |
| 20 | Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka. |
| 21 | Bali hii ni Qur'ani tukufu |
| 22 | Katika Ubao Ulio Hifadhiwa. |
| ReadTheQuran.org | |