| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
84 - AL - INSHIQAAQ | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Itapo chanika mbingu, |
| 2 | Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza, |
| 3 | Na ardhi itakapo tanuliwa, |
| 4 | Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu, |
| 5 | Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza, |
| 6 | Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta. |
| 7 | Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia, |
| 8 | Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi, |
| 9 | Na arudi kwa ahali zake na furaha. |
| 10 | Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake, |
| 11 | Basi huyo ataomba kuteketea. |
| 12 | Na ataingia Motoni. |
| 13 | Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake. |
| 14 | Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena. |
| 15 | Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona! |
| 16 | Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa, |
| 17 | Na kwa usiku na unavyo vikusanya, |
| 18 | Na kwa mwezi unapo pevuka, |
| 19 | Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka! |
| 20 | Basi wana nini hawaamini? |
| 21 | Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu? |
| 22 | Bali walio kufuru wanakanusha tu. |
| 23 | Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria. |
| 24 | Basi wabashirie adhabu chungu! |
| 25 | Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika. |
| ReadTheQuran.org | |