| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
82 - AL - INFIT'AAR | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Mbingu itapo chanika, |
| 2 | Na nyota zitapo tawanyika, |
| 3 | Na bahari zitakapo pasuliwa, |
| 4 | Na makaburi yatapo fukuliwa, |
| 5 | Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma. |
| 6 | Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? |
| 7 | Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha, |
| 8 | Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga. |
| 9 | Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo. |
| 10 | Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu, |
| 11 | Waandishi wenye hishima, |
| 12 | Wanayajua mnayo yatenda. |
| 13 | Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema, |
| 14 | Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni; |
| 15 | Wataingia humo Siku ya Malipo. |
| 16 | Na hawatoacha kuwamo humo. |
| 17 | Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? |
| 18 | Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? |
| 19 | Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu. |
| ReadTheQuran.org | |