| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
81 - ATTAKWIR | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Jua litakapo kunjwa, s |
| 2 | Na nyota zikazimwa, |
| 3 | Na milima ikaondolewa, |
| 4 | Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe, |
| 5 | Na wanyama wa mwituni wakakusanywa, |
| 6 | Na bahari zikawaka moto, |
| 7 | Na nafsi zikaunganishwa, |
| 8 | Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa, |
| 9 | Kwa kosa gani aliuliwa? |
| 10 | Na madaftari yatakapo enezwa, |
| 11 | Na mbingu itapo tanduliwa, |
| 12 | Na Jahannamu itapo chochewa, |
| 13 | Na Pepo ikasogezwa, |
| 14 | Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha. |
| 15 | Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma, |
| 16 | Zinazo kwenda, kisha zikajificha, |
| 17 | Na kwa usiku unapo pungua, |
| 18 | Na kwa asubuhi inapo pambazuka, |
| 19 | Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu, |
| 20 | Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi, |
| 21 | Anaye t'iiwa, tena muaminifu. |
| 22 | Na wala huyu mwenzenu hana wazimu. |
| 23 | Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi. |
| 24 | Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu. |
| 25 | Wala hii si kauli ya Shetani maluuni. |
| 26 | Basi mnakwenda wapi? |
| 27 | Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. |
| 28 | Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa. |
| 29 | Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
| ReadTheQuran.org | |