| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
78 - ANNABAA | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | WANAULIZANA nini? |
| 2 | Ile khabari kuu, |
| 3 | Ambayo kwayo wanakhitalifiana. |
| 4 | La! Karibu watakuja jua. |
| 5 | Tena la! Karibu watakuja jua. |
| 6 | Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko? |
| 7 | Na milima kama vigingi? |
| 8 | Na tukakuumbeni kwa jozi? |
| 9 | Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko? |
| 10 | Na tukaufanya usiku ni nguo? |
| 11 | Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha? |
| 12 | Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu? |
| 13 | Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto; |
| 14 | Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni, |
| 15 | Ili tutoe kwayo nafaka na mimea, |
| 16 | Na mabustani yenye miti iliyo kamatana. |
| 17 | Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake, |
| 18 | Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi, |
| 19 | Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango, |
| 20 | Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi. |
| 21 | Hakika Jahannamu inangojea! |
| 22 | Kwa walio asi ndio makaazi yao, |
| 23 | Wakae humo karne baada ya karne, |
| 24 | Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji, |
| 25 | Ila maji yamoto sana na usaha, |
| 26 | Ndio jaza muwafaka. |
| 27 | Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu. |
| 28 | Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu. |
| 29 | Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika. |
| 30 | Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu! |
| 31 | Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu, |
| 32 | Mabustani na mizabibu, |
| 33 | Na wake walio lingana nao, |
| 34 | Na bilauri zilizo jaa, |
| 35 | Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo - |
| 36 | Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha. |
| 37 | Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake! |
| 38 | Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu. |
| 39 | Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi. |
| 40 | Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo! |
| ReadTheQuran.org | |