Translations Suras
KISWAHILI

75 - AL - QIYAMAH

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!
 
2Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu!
 
3Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
 
4Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!
 
5Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake.
 
6Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?
 
7Basi jicho litapo dawaa,
 
8Na mwezi utapo patwa,
 
9Na likakusanywa jua na mwezi,
 
10Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?
 
11La! Hapana pa kukimbilia!
 
12Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.
 
13Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha.
 
14Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.
 
15Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.
 
16Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.
 
17Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.
 
18Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.
 
19Kisha ni juu yetu kuubainisha.
 
20Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani,
 
21Na mnaacha maisha ya Akhera.
 
22Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara,
 
23Zinamwangallia Mola wao Mlezi.
 
24Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana.
 
25Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.
 
26La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo,
 
27Na pakasemwa: Nani wa kumganga?
 
28Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki;
 
29Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi,
 
30Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi!
 
31Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali.
 
32Bali alikanusha, na akageuka.
 
33Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao.
 
34Ole wako, ole wako!
 
35Kisha Ole wako, ole wako!
 
36Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure?
 
37Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?
 
38Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.
 
39Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.
 
40Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?
 
 
ReadTheQuran.org