| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
56 - AL -WAAQIA'H | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Litakapo tukia hilo Tukio |
| 2 | Hapana cha kukanusha kutukia kwake. |
| 3 | Literemshalo linyanyualo, |
| 4 | Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso, |
| 5 | Na milima itapo sagwasagwa, |
| 6 | Iwe mavumbi yanayo peperushwa, |
| 7 | Na nyinyi mtakuwa namna tatu:- |
| 8 | Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani? |
| 9 | Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni? |
| 10 | Na wa mbele watakuwa mbele. |
| 11 | Hao ndio watakao karibishwa |
| 12 | Katika Bustani zenye neema. |
| 13 | Fungu kubwa katika wa mwanzo, |
| 14 | Na wachache katika wa mwisho. |
| 15 | Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa. |
| 16 | Wakiviegemea wakielekeana. |
| 17 | Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele, |
| 18 | Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi. |
| 19 | Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa. |
| 20 | Na matunda wayapendayo, |
| 21 | Na nyama za ndege kama wanavyo tamani. |
| 22 | Na Mahurulaini, |
| 23 | Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa. |
| 24 | Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda. |
| 25 | Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi, |
| 26 | Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama. |
| 27 | Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani? |
| 28 | Katika mikunazi isiyo na miba, |
| 29 | Na migomba iliyo pangiliwa, |
| 30 | Na kivuli kilicho tanda, |
| 31 | Na maji yanayo miminika, |
| 32 | Na matunda mengi, |
| 33 | Hayatindikii wala hayakatazwi, |
| 34 | Na matandiko yaliyo nyanyuliwa. |
| 35 | Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya, |
| 36 | Na tutawafanya vijana, |
| 37 | Wanapendana na waume zao, hirimu moja. |
| 38 | Kwa ajili ya watu wa kuliani. |
| 39 | Fungu kubwa katika wa mwanzo, |
| 40 | Na fungu kubwa katika wa mwisho. 3 |
| 41 | Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni? |
| 42 | Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka, |
| 43 | Na kivuli cha moshi mweusi, |
| 44 | Si cha kuburudisha wala kustarehesha. |
| 45 | Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa. |
| 46 | Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa, |
| 47 | Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa? |
| 48 | Au baba zetu wa zamani? |
| 49 | Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho |
| 50 | Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu. |
| 51 | Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha, |
| 52 | Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu. |
| 53 | Na kwa mti huo mtajaza matumbo. |
| 54 | Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka. |
| 55 | Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu. |
| 56 | Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo. |
| 57 | Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki? |
| 58 | Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza? |
| 59 | Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji? |
| 60 | Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi |
| 61 | Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua. |
| 62 | Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki? |
| 63 | Je! Mnaona makulima mnayo yapanda? |
| 64 | Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha? |
| 65 | Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu, |
| 66 | Mkisema: Hakika sisi tumegharimika; |
| 67 | Bali sisi tumenyimwa. |
| 68 | Je! Mnayaona maji mnayo yanywa? |
| 69 | Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha? |
| 70 | Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru? |
| 71 | Je! Mnauona moto mnao uwasha? |
| 72 | Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji? |
| 73 | Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani. |
| 74 | Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu. |
| 75 | Basi naapa kwa maanguko ya nyota, |
| 76 | Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua! |
| 77 | Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu, |
| 78 | Katika Kitabu kilicho hifadhiwa. |
| 79 | Hapana akigusaye ila walio takaswa. |
| 80 | Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
| 81 | Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza? |
| 82 | Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha? |
| 83 | Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo, |
| 84 | Na nyinyi wakati huo mnatazama! |
| 85 | Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi. |
| 86 | Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu, |
| 87 | Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli? |
| 88 | Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa, |
| 89 | Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema. |
| 90 | Na akiwa katika watu wa upande wa kulia, |
| 91 | Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia. |
| 92 | Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu, |
| 93 | Basi karamu yake ni maji yanayo chemka, |
| 94 | Na kutiwa Motoni. |
| 95 | Hakika hii ndiyo haki yenye yakini. |
| 96 | Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa. |
| ReadTheQuran.org | |