| Translations | Suras |
| KISWAHILI | |
55 - ARRAH'MAN | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
| 1 | Arrah'man, Mwingi wa Rehema |
| 2 | Amefundisha Qur'ani. |
| 3 | Amemuumba mwanaadamu, |
| 4 | Akamfundisha kubaini. |
| 5 | Jua na mwezi huenda kwa hisabu. |
| 6 | Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea. |
| 7 | Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani, |
| 8 | Ili msidhulumu katika mizani. |
| 9 | Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani. |
| 10 | Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe. |
| 11 | Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba. |
| 12 | Na nafaka zenye makapi, na rehani. |
| 13 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha |
| 14 | Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo.. |
| 15 | Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto. |
| 16 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha |
| 17 | Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili. |
| 18 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 19 | Anaziendesha bahari mbili zikutane; |
| 20 | Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane. |
| 21 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 22 | Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani. |
| 23 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 24 | Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima. |
| 25 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 26 | Kila kilioko juu yake kitatoweka. |
| 27 | Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu. |
| 28 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 29 | Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo. |
| 30 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 31 | Tutakuhisabuni enyi makundi mawili. |
| 32 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 33 | Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka. |
| 34 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 35 | Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda. |
| 36 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 37 | Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta. |
| 38 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 39 | Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini. |
| 40 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 41 | Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu. |
| 42 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 43 | Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha. |
| 44 | Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka. |
| 45 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 46 | Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili. |
| 47 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 48 | Bustani zenye matawi yaliyo tanda. |
| 49 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 50 | Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita. |
| 51 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 52 | Humo katika kila matunda zimo namna mbili. |
| 53 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 54 | Wawe wameegemea matandiko yenye bit'ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu. |
| 55 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 56 | Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini. |
| 57 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 58 | Kama kwamba wao ni yakuti na marijani. |
| 59 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha. |
| 60 | Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani? |
| 61 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 62 | Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili. |
| 63 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 64 | Za kijani kibivu. |
| 65 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 66 | Na chemchem mbili zinazo furika. |
| 67 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 68 | Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga. |
| 69 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 70 | Humo wamo wanawake wema wazuri. |
| 71 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 72 | Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema. |
| 73 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 74 | Hajawagusa mtu wala jini kabla yao. |
| 75 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 76 | Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri. |
| 77 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
| 78 | Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu. |
| ReadTheQuran.org | |