Translations Suras
KISWAHILI

1 - AL-FAATIH'A

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
 
2Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;
 
3Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu;
 
4Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo.
 
5Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.
 
6Tuongoe njia iliyo nyooka,
 
7Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.
 
 
ReadTheQuran.org